Uyui FM Radio

Serikali kuboresha viwanja vya nanenane Tabora

9 August 2024, 9:07 pm

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye maonesho.Picha na Mohamed Habibu

Kaulimbiu ya maonesho ya nane nane mwaka huu ni ‘’Chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Na Zaituni Juma

Serikali  imewaagiza waratibu wa maonesho ya nane nane kanda ya magharibi kuandaa mpango mahususi wa matumizi ya viwanja vya maonesho hayo ili kuwavutia wawekezaji kujenga majengo ya kudumu.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema hayo wakati akiwa viwanja vya Ipuli mnadani Manispaa ya Tabora  kwenye kilele cha maonesho ya nane nane Kanda ya magharibi.

Mkuu wa mkoa wa Tabora akizungumza na wananchi.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Paul Chacha

Awali akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Kigoma ambae ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina amesema kilimo,ufugaji na uvuvi ni sekta muhimu katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Kanali Michael Ngayalina.Picha na Mohamed Habibu
Sauti Kanali Ngayalina

Katika washindi , Tabora Manispaa imekuwa mshindi wa tatu,mshindi wa pili ni wilaya ya Igunga na Kigoma ujiji imeibuka mshindi wa kwanza.