Uyui FM Radio

Sekta ya kilimo ni mwarobaini wa ajira-Zitto Kabwe

6 August 2024, 1:37 pm

Baadhi ya wanachama na wananchi wakiwa kwenye mkutano.Picha na Mohamed Habibu

Kiongozi mstaafu wa ACT wazalendo ZITTO KABWE  yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku 6  ambayo imelenga kutangaza sera za chama hicho.  

Na Zaituni Juma

Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo ZITTO KABWE amesema ili kuleta maendeleo ni lazima kuwekeza  kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya kilimo.

Zitto amesema hayo akiwa mkoani  Tabora kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya CHEMCHEM ambapo amesema endapo uwekezaji mkubwa ukifanyika kwenye kilimo utasaidia vijana wengi kupata ajira.

Zitto akizungumza na wanachama pamoja na wananchi.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Zitto Kabwe

Awali katibu wa ACT Wazalendo mkoa wa Tabora Hamis Mahanga ametaja changamoto kwa baadhi ya vijana kufanya kazi za aina moja bila kupata manufaa makubwa.

Katibu wa ACT Wazalendo Tabora Hamis Mahanga akizungumza.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Hamisi Mahanga