Uyui FM Radio
Bilioni 26 kutengeneza barabara mkoani Tabora
22 July 2024, 6:15 pm
TARURA mkoa wa Tabora anasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilolemta 8,404 .
Na Zaituni Juma
Jumla ya shilingi bilioni 26 zimetengwa na serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwaajili ya kutengeneza barabara katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora.
Meneja wa wakala ya barabara za vijijini na mijini TARURA mkoa wa Tabora Mhandisi LUSAKO KILEMBE amesema hayo wakati akizungumza na UFR.
Kwa upande wake meneja wa TARURA wilaya ya Tabora Mhandisi Vicent Manyama ambae pia ni mratibu wa mradi wa benki ya dunia wilayani humo ametaja barabara za mitaa ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami.