Uyui FM Radio

23 mbaroni tuhuma za udanganyifu wa ajira kwa vijana

12 July 2024, 6:32 pm

Watuhumiwa wakiwa kwenye gari la polisi.Picha na Salma Abdul

Kwa mujibu wa taarifa vijana hao zaidi ya 100 walipigiwa simu kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Singida, Dodoma na Morogoro kuja mkoani Tabora kwa lengo la kuwapatia ajira zenye mshahara mnono

Na Salma Abdul

Watu 23 ambao ni baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Alliance in Motion Global, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani Tabora kwa tuhuma za kufanya udanganyifu kwa vijana zaidi ya 100 kuwapatia ajira.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Deusdedit Katwale amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kubaini kuwa vijana hao wanahangaika baada ya kutapeliwa.

Dc Katwale akizungumza na viongozi wa Kampuni na vijana.Picha na Salma Abdul
Sauti ya DC Katwale

Awali wakielezea adha walioipata baadhi ya vijana hao wameiomba serikali kuwasaidia nauli ili warudi nyumbani kwao.

mmoja wa vijana Arafa Issa akizungumza na waandishi.Picha na Salma Abdul

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Tabora Katwale amezitaka Taasisi na Kampuni mbalimbali kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ikiwemo kufanya kazi wakiwa na leseni.

Mkuu wilaya Katwale ameagiza viongozi wa kambi zote zilizokuwa zikiendesha mafunzo kwa vijana hao kuwarudishia nauli wahusika ili warejee kwenye mikoa wanayoishi.