Shekhe asimamishwa kwa kuratibu ndoa bandia
12 July 2024, 5:14 pm
Suala hilo limetokea kutokana na mpango wa mfadhili kuwatafuta vijana kwa lengo la kuwafungisha ndoa na kugharamia mahari pamoja na mambo mengine.
Na Zaituni Juma
Baraza la Mashehe mkoani Tabora limemsimamisha kazi Shekhe wa kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora Bakari Sikonge, kwa kukiuka maadili na kuratibu ndoa kwa mtu ambaye tayari alishafunga ndoa awali.
Akizungumzia suala hilo Shekhe wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amesema kuwa mbali na kusimamishwa pia wataendelea kufuatilia mienendo yake ili kujiridhisha kama amebadilika au la.
Amesisitiza kuwa baraza litaendelea kufuatilia mienendo ya viongozi hao na endapo itabainika kuwa wana mengine wanayofanya kinyume na maelekezo hatua za kinidhamu zitachuliwa dhidi yao.