Serikali yatoa onyo kwa wenye vibali uvunaji mazao ya misitu
18 June 2024, 4:46 pm
Operesheni hiyo ya kufuatilia wanaokiuka taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Uyui imeanza wiki ya mazingira Mei 29 mwaka huu ikiwa na kaulimbiu isemayo ‘’urejeshwaji wa ardhi iliyoharibiwa, ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame’’
Na Zaituni Juma
Jumla ya magari matano yamekamatwa wilayani Uyui mkoani Tabora yakiwa na zaidi ya magunia ya mkaa 200, mbao pamoja na nguzo kwa kukiuka taratibu za vibali na uvunaji wa mazao ya misitu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Uyui Zakaria Mwansasu amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka utaratibu.
Pia mkuu wa wilaya Mwansasu ameagiza wakala wa misitu Tanzania-TFS wilaya ya Uyui kufanya kazi kwa weledi bila kumuogopa mtu yoyote.
Muhifadhi misitu wilaya ya Uyui Majaliwa Maginga amesema watahakikisha wanafanya doria za mara kwa mara ili kuwabaini na kuwakamata wanaokiuka sheria.