Afisa maendeleo-Msiwatelekeze watoto kwa bibi na babu zao
12 June 2024, 11:58 am
Kila ifikapo juni 12 ya kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya kupinga utumikishwaji wa Mtoto ambapo kwa mwaka huu imebeba kaulimbiua isemayo ‘’komesha utumikishwaji wa mtoto’’
Na Zaituni Juma
Wazazi na walezi wilayani Tabora wameaswa kutowatelekeza watoto wao kwa wazee suala linalochangia kwa kiasi kikubwa utumikishwaji kwenye maeneo mbalimbali.
Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Tabora Helena Mathias amseema hayo wakati akizungumza na UFR ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga utumikishwaji wa mtoto duniani ambayo kimkoa yanafanyika kijiji cha Kalemela ‘B’ wilayani Urambo.
Kwa upande wake Afisa mradi wa Taasisi ya Elimu bora Foundaution mwalimu Grace Kasoga amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa walimu mashuleni ili kuzingatia utoaji wa adhabu kwa wanafunzi.
Nae mhamasishaji wa shirika lisilo la kiserikali lilipo mkoani Tabora –CODEWA Happy Kitanga ameeleza mojawapo ya sababu za utumikishwaji wa watoto.