”Wananchi toeni taarifa za uhalifu kwasababu Polisi ni wachache” -DCP Nzuki
4 August 2023, 3:46 pm
Wananchi wameombwa kufichua taarifa za wahalifu kufuatia kuwepo kwa idadi ndogo ya askari Polisi.
Na Salma Abdul.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Maria Nzuki ameomba ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu kwa Jeshi la Polisi kufuatia kuwepo kwa idadi ndogo ya askari Polisi
Amsema hayo akiwa kwenye tarafa ya Manonga kata ya Nyandekwa kijiji cha Usongo Wilayani Igunga Mkoani Tabora
Vile vile amekagua vikundi vya Sungu Sungu, na kushuhudia igizo ambalo limeonesha namna Sungu sungu wanavyofanya kazi Kwa kuzingatia sheria baada ya kupata elimu ya Polisi jamii.
Katika kikao hicho Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa polisi Richard Abwao amewahimiza wenyeviti wa vitongoji kuwa na madaftari yenye taarifa za watu wanaoishi maeneo yao ili kuzuia uhalifu.
Hata hivyo Naibu kamishna amevikwa Utemi wa kabila la wasukuma wilayani Igunga mkoani Tabora na kupewa jina la GINDU NKIMA.