Wakulima Kanda ya Magharibi watakiwa kushiriki maonesho ya nanenane
4 August 2023, 3:15 pm
Mkuu wa mkoa wa Tabora amesema maonesho ya nane nane yanalenga kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo bora.
Na Omary Khamis
Wakulima kanda ya magharibi wametakiwa kushiriki maonesho ya nanenane ili kujifunza mbinu bora zitakazo wasaidia kuvuna mazao mengi na kupata kipato zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Daktari Batilda Buriani ameyasema hayo akiwa ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliotembelea maonesho ya hayo katika viwanja vya Fatma Mwasa vilivyopo- Ipuli Manispaa ya TABORA Asha Bakari na Deogratias Kaswiza wameelezea sababu inayosababisha kuuuza mazao yao kabla ya msimu ikiwa ni pamoja na uhakika wa masoko.
Maadhimisho ya siku ya wakulima duniani ambayo hufanyika kuanzia tarehe moja hadi tarehe nane mwezi wa nane kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo ‘’vijana na wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”