Zaidi ya bilioni moja kujenga shule za msingi Tabora
3 July 2023, 12:22 pm
Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1 na milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi kwenye kata za Mtendeni, Mbugani na Tambukareli manispaa ya Tabora ili kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa katika manispaa hiyo.
Na Zaitun Juma
Hayo yamebainishwa na mstahiki meya manispaa ya Tabora Ramdhani Kapela ambaye amesema mbali na kuboresha miundombinu ya elimu pia miradi hiyo inachochea maendeleo kwenye kata husika kupitia ajira.
Akizungumzia ujenzi wa shule mpya ya msingi Mabatini, afisa mtendaji kata ya Tambukareli Hussein Majimoto amesema kwa sasa upo katika hatua ya upauaji.
Kwa mujibu wa afisa mtendaji Majimoto amesema ujenzi wa shule mpya ya msingi Mabatini ambao umejumuisha madarasa 7,ofisi moja na shule ya awali ya mfano utaondoa changamoto ya upungufu wa madarasa uliopo.