Watoa huduma za mawasiliano Kanda ya kati wanolewa juu ya UCSAF
19 May 2021, 7:21 pm
Watoa huduma za mawasiliano katika mkoa wa Tabora, singida na Kigoma wametakiwa kuwa na ushirikiano kwa wananchi ili kutumia mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF kwa lengo la kuhakikisha huduma inayotolewa inakuwa bora hususani katika maeneo ya vijijini.
RICHARD SOTERY ni Mhandisi Kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote amesema hayo katika mkutano wa wadau wa mawasilino kutoka mikoa mitatu ambayo ni Tabora, Kigoma na singida mkutano uliofanyika mjini HAPA.
Kwa upande wao baadhi ya wadau wa huduma za mawasiliano walioshiriki kwenye mkutano huo JAMES JAPHET, na ELISHEBAN BENEYE wamesema licha ya kuchelewa kwa upatikanaji wa elimu kwa watoa huduma za mawasiliano wameutaka mfuko huo kuwekeza zaidi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za mawasiliano.
JOSEPH KAVISHE ni AFISA SHERIA kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania amesema kuwa kuna ushirikiano kati ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania na mfuko wa mawasiliano kwa wote ili kuongeza kasi ya upelekaji wa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa umma ambapo amewasisitiza watoa huduma kuzingatia taratibu zilizopo.