Wananchi Kaliua wapigwa marufuku hifadhi ya Isawima.
12 April 2021, 5:49 pm
Naibu waziri wa maliasiri na utalii Marry Masanja amezuia wananchi kufanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi ya ISAWIMA wilayani Kaliua mkoani Tabora baada ya wananchi kuvamia hifadhi hiyo na kukaidi maelekezo ya serikali ya mkoa iliyowataka kuondoka.
Naibu waziri amesema wananchi ambao tayari wamefanya shughuli za kilimo ndani ya hifadhi watapewa kibali cha kuvuna mazao lakini usiwepo mwendelezo wa aina yoyote ya shughuli za kibinadamu.
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa wilaya ya kaliua wameiomba serikali kuwarekebishia mipaka ilIyopo kati ya Kijiji cha ACHA WASEME kwani wamekuwa wakitegemea maeneo hayo kwaajili ya kujipatia riziki yao.
Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kaliua ABELI BUSALAMA amesema tangu mwaka 2017 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati daktari JOHN POMBE MAGUFULI aliwapa eneo wananchi hao walioingi ndani ya hifadhi hiyo ya Isawima kwa lengo la kuacha kuingia kwenye hifadhi kwa kufanya makazi na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo.