Wananchi Tabora waendelea kumuenzi Dkt. Magufuli
24 March 2021, 1:14 pm
Jamii katika Manispaa ya Tabora imesema inamuenzi na itaendelea kumkumbuka aliyekuwa Raisi wa awamu ya tano katika Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa juhudi na uchapakazi wake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za kijamii.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakaazi wa Manipsaa ya Tabora waliofika na kusaini kitabu cha maombolezo cha hayati Dkt John Magufuli katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora .
Christopha David,Husein Katanga na Gorge Nsunzu ambao ni baadhi ya wananchi hao wamesema hayati Dkt Magufuli alikuwa mchapakazi aliyelenga matokeo chanya katika utendaji kazi wake.
Insert…wananchi….dak…1
Akizungumzia namna ambavyo Hayati Dkt john Mahufuli alivyo watumikia wanachi enzi za uhai wake,Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi mkoa wa Tabora Marselina Mpandachalo amesema huduma za afya zimeboreshwa huku akiahidi kushirikiana na Rais mpya wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassani.
Insert…..mpandachalo……dak…2