Radio Jamii Kilosa

Kilosa bila mimba za utotoni inawezekana, tuwalinde

10 September 2024, 1:00 am

Mtoa huduma wa ngazi za jamii na mabinti kituo cha afya Kimamba Bi Mariam Kamala. Picha na Aloycia Mhina

Na Aloycia Mhina

Mimba za utotoni ni suala linalohitaji umakini mkubwa kutokana na athari zake kwa afya ya mama na mtoto, ambapo Mariamu Kamala mtoa huduma ngazi za jamii na mabinti katika kituo cha afya Kimamba amesema athari zake ni pamoja na vifo kutokana na matatizo ya shinikizo la damu hatari na matatizo ya kujifungua.

Amesema kuwa matatizo ya afya kwa mama mjamzito ni tatizo kubwa kiafya na kwamba madhara ni mengi kutokana na mabinti kuwa na tamaa, na kuwataka wazazi wakae vizuri na mabinti zao wafahamu changamoto zao katika maisha yao.

“Katika kituo cha Afya kata ya Kimamba Wilayani Kilosa mimba za utotoni zimekuwa ni changamoto sana kwa watoto wa kike wenye umri mdogo na tumekuwa tukipambana na mabinti hawa katika kituo chetu cha Afya” alisema Bi Mariam.

Sauti ya Bi Mariam Kamala

Maua Haridi anasema alipata mimba ya utotoni akiwa na miaka {!15] mara baada ya wazazi wake kumuozesha katika umri huo mdogo anaeleza namna aliivyopitia changamoto mbalimbali baada ya mwanaume aliyefunga naye ndoa ya utotoni na kumuacha na ujauzito

Sauti ya mhanga Bi Maua Haridi

Naye Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wilayani Kilosa Priska John amesema Kilosa ina asilimia 24 ya mimba za utotoni kwa kipindi cha mwaka jana mbali ya hiyo zipo kesi za wanafunzi waliokatisha masomo yao kutokana na ujauzito na kwamba kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hasa mimba na ndoa za utotoni itasaidia kuwafanya watoto wa kike kufikia malengo yao ya maisha.