Radio Jamii Kilosa

Wanahabari Kilosa waaswa kuzingatia ukweli, haki na usawa

8 May 2024, 5:27 pm

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Alexander Ruhundwa kushoto akiwa katika studio za Redio Jamii Kilosa. Picha na Happy Luoga

Mitandao ya kijamii inachangia kwa kiasi kikubwa kuifikia jamii kubwa katika kuwahabarisha, kuwaunganisha na kudumisha upendo na amani hivyo wajibu kwa waandishi kuwa na weledi ya kutosha katika kuitumia mitandao hiyo.

Na Asha Madohola

Waandishi wa habari wa Redio Jamii Kilosa wametakiwa kutumia taaluma yao ili kuisaidia jamii katika kukabiliana na changamoto walizonazo kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Kauli hiyo ilitolewa na Mhariri kutoka Radio Tadio Hilali Alexander Ruhundwa kwenye mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika katika kituo cha redio hiyo ambapo alisema Radio Tadio ni mtandao wa redio za kijamii nchini unaorahisisha habari za redio washiriki kuwafikia watu wengi zaidi tofauti na habari zikiishia redioni kwa masafa ya kawaida.

Sauti ya Mhariri Radio Tadio Hilali Ruhundwa
Waandishi wa habari wa Redio Jamii Kilosa wakifuatilia mafunzo namna ya kushiriki habari katika mitandao ya kijamii.

Ruhundwa amesema kuwa waandishi wa redio washiriki wa Radio Tadio wanafanya vizuri zaidi kwenye uandishi kutokana na mafunzo ambayo wamekuwa wakiyatoa mara kwa mara ya kuwajengea uwezo ambapo habari zao hudika ulimwenguni kote.

Sauti ya Mhariri Hilali Ruhundwa

Aidha Ruhundwa amesema kuwa kuelekea vipindi vya chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia maadili ambayo yanawataka kuzingatia ukweli, haki na usawa ili kuleta matokeo chanya kwa jamii na kuepuka makundi ama kuegemea upande mmoja. Amewaasa wanahabari kuhakikisha wanaihabarisha jamii pasipo kuigawa na kuitumia mitandao ya kijamii katika kuhabarisha na kuburudisha.

Sauti ya Mhariri Hilali Ruhundwa

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Redio Jamii Kilosa, Meneja wa Redio Glady’s Mapeka ameishukuru Tadio kwa kuwezesha mafunzo hayo na kwamba wamejifunza mengi na ameahidi watayafanyia kazi ili kuleta tija kwa jamii inayowazunguka.

“Yapo mengine tulikuwa hatuyajui na mengi tuliyasahau lakini kupitia mafunzo haya yameweza kutukumbusha wajibu na misingi ya taaluma yetu ya habari hususani matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuhabarisha” amesema Mapeka.

Sauti ya Meneja wa Redio Jamii Kilosa Glady’s Mapeka
Hilali Ruhundwa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo