Loliondo FM
Loliondo FM
9 October 2026, 10:37 am

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), atembelea Ngorongoro na kuongoza tathmini ya uwezekano wa kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya.
Na Zacharia James
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amewasili Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha, kwa ziara ya kikazi inayolenga kutathmini uwezekano wa kujenga Kituo cha Huduma za Forodha katika Kijiji cha Njoroi, eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya.Hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za mpakani, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuimarisha usalama wa nchi na kurasimisha shughuli za biashara pamoja na taratibu za uhamiaji katika eneo hilo.
Akieleza umuhimu wa tathmini hiyo, Mhe. Munde amesema kuwa Serikali imeamua kuwashirikisha wataalamu ili kuchunguza mahitaji na mazingira ya eneo la Njoroi kabla ya kufanya maamuzi kuhusu ujenzi wa kituo hicho.Uwezekano wa kuanzishwa kwa kituo hicho unaweka mbele umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti ya usimamizi wa shughuli za mpakani, itakayosaidia kudhibiti mienendo ya watu na bidhaa, kupunguza mianya ya upotevu wa mapato na kuimarisha utekelezaji wa sheria na taratibu za nchi.
Kwa upande wake mbunge wa ngorongoro mhe yannick ndoinyo amesema kilichomsukuma kupeleka ombi hilo kwa serikali kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya ngorongoro ni kutokana na msukumo mkubwa wa wilaya ya ngorongoro kutaka kukua kiuchumi kupitia fulsa nyingi za vitega uchumi,biashara ya mifugo inayofanyika katika eneo hilo,ukuaji wa wa haraka wa mji huo kuanzia miaka saba iliopita na muingiliano wa idadi kubwa ya watu kati ya tanzania na kenya mambo ambayo mhe mbunge ameyaelezea kuwa yanahitaji usimamizi madhubuti ambapo kwa kujenga kituo cha forodha,uhamiaji na vituo vingie vya kuchochea biashara
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Manja Sironga Yaile, ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza ushuru unaotozwa katika shughuli za uuzaji na ununuzi wa mifugo, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kurahisisha biashara na kuongeza kipato cha wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa mifugo.Mhe. Yaile amesema kuwa biashara ya mifugo ni miongoni mwa shughuli muhimu za kiuchumi kwa wananchi wa Ngorongoro, hivyo kuna umuhimu wa kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wafugaji na wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa urahisi na kupata manufaa zaidi kutokana na mifugo yao.