Loliondo FM

Makala: Ukatili wa kijinsia ni kinyume na Haki za binadamu

8 December 2023, 10:50 am

Manusura wa ukatili wa kijinsia wakiwa katika nyumba salama ya Mimutie girls rescue center

Watoto wa kike kutoka jamii za kimaasai wanaeendelea kuwa wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia

Na Saitoti Saringe

Kutokana na mila kandamizi katika jamii ikiwemo ukeketaji, kutopewa fursa ya elimu na kumiliki ardhi ni sababu kubwa inayopelekea watoto wengi kutoka katika jamii hizi kutofikia ndoto zao

Baadhi ya jamii zimeendelea kushikilia mila kandamizi ambapo imeendelea kudidimiza jitihada za serikali na wadau wengine katika kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii suala linalopelekea ukatili kuwa tishio ndani ya jamii.

Karibu kusikiliza makala maalum iliyoandaliwa na Saitoti Saringe kwa ushirikiano na shirika la Mimutie Women Organization ikiangazia juu ya athari za ukatili wa kijinsia katika jamii za pembezoni.

kusikiliza makala hii bonyeza hapa