Loliondo FM

Hakimu atumia pombe kumlawiti dereva bodaboda Loliondo

6 February 2024, 3:41 pm

l

Picha na mtandao

Matukio ya ulawiti yamekuwa ayatendeki kwa kiasi kikubwa na viongozi wa utoaji haki kwani imekuwa ni mara chache  kusikia yakiripotiwa na hukumu zikitolewa huku kwa wilaya ya Ngorongoro likiwa ni tukio la kwanza kuripotiwa la hakimu kutuhumiwa kutenda kosa la ulawiti.

Na Edward Shao

Hakimu wa mahakama ya mwanzo wilayani Ngorongoro Benson Ngowi (32) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutenda kosa la kumlawiti dereva bodaboda mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa mji mdogo wa Wasso siku ya Ijumaa ya Februari 02, 2024  akidaiwa kuleweshwa pombe kisha kufanyiwa kitendo hicho.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro  Kanali Wilson Sakulo amesema amezipata taarifa za hakimu huyo na jeshi la polisi limeshikilia kwa uchunguzi kubaini undani wake huku akitaja kuwa, vitendo vya ulawiti ni mojawapo ya ukatili na  mtu yeyote anayefanya vitendo hivyo akibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya

Kwa mujibu wa mashuuda wa tukio hilo mtuhiwa alikuwa nyumbani kwa kijana huyo wakinywa pombe kwa pamoja ndipo baadae kaka wa kijana huyo ilipogundua hakimu huyo ametenda tukio la kumuingilia kinyume na maumbile mdogo wake.