Loliondo FM

Auawa kwa kuchapwa na mume wake akilazimishwa kuishi nae Ngorongoro

10 February 2024, 1:36 pm

PWC,ustawi wa jamii Ngorongoro wakiwa na mama wa marehemu katikati,picha na Edward Shao.

Matukio ya ukatili kwa wanawake yameendela kuripotiwa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 22 auawa kwa kuchapwa na mume wake akilazimishwa kuishi nae Ngorongoro.

Na Edward Shao.

Mwanamke mmoja Nanyori Mohe (22) mkaazi wa kijiji cha Malambo kata ya Malambo wilayani Ngorongoro ameauawa kwa kuchapwa na mume wake akilazimishwa kuishi nae.

Shirika la PWC linalotetea haki za wanawake wakiambata na afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro bi Steya Melubo limemtembea mama wa binti aliyeuawa kwa kipigo na mume wake katika kitongoji cha Madukani kijiji cha Malambo kata ya Malambo wilayani Ngorongoro baada ya kugoma kuishi nae kwa muda wa miaka 3 licha ya kufunga ndoa ya kimila mwaka 2020.

Tukio hilo limetokea siku ya tarehe 6 Februari 2024 Kijijini hapo ambapo mtuhumiwa Lanyori Mathayo (25) alienda kumfata nyumbani kwa wazazi wa marehemu Nanyori Mohe (22) alikokuwa siku ya tukio na kuondoka nae hadi pori lilopo jirani na nyumbani kwa mtuhumiwa kisha kumfunga kamba miguuni na mikononi Kisha kumfunga kwenye mti ndipo alipoanza kumtandika kwa kutumia waya wa umeme aliokuwa nao.

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Malambo bwn. Lameck Lucas amesema walimpokea mgonjwa tarehe 7 Februari 2024 saa nne kuelekea saa tano asubuhi akiwa na hali mbaya na majeraha makubwa yakuchapwa na fimbo maeoneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo mgongoni,mikononi,kifuani na kichawani.

Sauti ya mganga mfawidhi

Baba wa marehemu Bwn Mathayo Mohe pamoja na mume wa marehemu aliyetenda ukatili huo Bwn Lanyori Mathayo wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani hapa.

Alipotafutwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo kuzungumzia tukio hilo simu yake iliita bila mafanikio.