Loliondo FM

Serikali yakabidhi vifaa vya wanafunzi wenye huitaji maalum Ngorongoro

16 January 2024, 11:33 pm

Picha ya Emanuel Mhando kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mhando akiwa na Madam Mwanamina Muro afisa elimu awali na msingi wilaya, Mwl. Ronald Mwende afisa elimu maalum wilaya, pamoja na mwl Hamad Lesso mkuu wa shule ya msingi Endulen.

Serikali imeendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowafanya wanafunzi kushindwa kuendelea na na masomo ikiwemo kutoa vifaa vya kusomea kwa wanafunzi wenye huitaji maalum.

Na Edward Shao.

Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro imepokea vifaa maalum kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania imeendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu nchini kwa kutoa vifaa maalum vitakavyokwenda kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Endulen iliyopo wilayani Ngorongoro.

Aidha vifaa hivyo vimepokelewa katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jumatatu ya Januari 15,2024 na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri bw. Emmanuel Mhando akiwa na madam Mwanamina Muro afisa elimu awali na msingi wilaya, mwl. Ronald Mwende afisa elimu maalum wilaya, pamoja Mwl. Hamad Lesso mkuu wa shule ya msingi Endulen.

Hata hivyo bw. Emmanuel Mhando kwaniaba ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kutoa vifaa hivi maalum kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwani vinakwenda kuleta tija kubwa katika sekta ya elimu hapa nchini.

Ikumbukwe lengo la vifaa hivi ni kuchochea maendeleo ya wenye mahitaji maalum katika ufaulu, kutokomeza utoro pia kuimarisha na kuboresha sekta ya elimu maalum wilaya ya Ngorongoro.