Loliondo FM

Kamati ya siasa Arusha yaridhishwa miradi ya maendeleo Ngorongoro

8 March 2024, 11:03 am

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha katikati Ndg , Loy Ole Sabaya akiwa na viongozi mbalimbali wilayani Ngorongoro.

Ni ziara ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiambatana na viongozi wengine wa mkoa ikiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha Mh John Mongella wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani hapa huku wakitoa pongezi kwa mkurugenzi mtendaji kwa halmashauri ya Ngorongoro kwa kazi kubwa yakusimamia miradi inayoendelea kutekelezwa wilayani hapa.

Na mwindishi wetu.

Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro chini ya Bw. Nassoro Shemzigwa, imeendelea kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Mhe. rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Mhe. Loy Ole Sabaya leo tarehe 4 Machi, 2024 ameiongoza kamati ya siasa ya mkoa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa wilayani Ngorongoro, na kutoa pongezi kwa miradi inayoridhisha katika utekelazwaji ikiwemo shule ya sekondari Masusu ambayo imekamilika kisha kutoa maagizo ya ukamilishwaji kwa miradi yote ili kuhakikisha utendaji kazi unaenda vizuri na miradi inakamilika kwa wakati.

Aidha Mwenyekiti ametoa pongezi kwa Wananchi wa Kata ya Pinyinyi na Uongozi wa Halmashauri kwa juhudi walizozifanya kuhakikisha Shule ya Sekondari Masusu inakamilika.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha

Shule ya Masusu imegharimu kiasi cha shilingi milion 584.2, Shule hiyo ina madarasa 8, ofisi 2, jengo la utawala, maabara ya kemia, fizikia, baiolojia, jengo moja la maktaba na jengo la tehama.