Loliondo FM

Mbunge Ole Shangai awaka sakata la uhamaji wa hiari Ngorongoro

9 April 2024, 11:17 am

Mbunge wa jimbo la Ngorongoro mh Emanuel Lekishon Ole Shangai, picha na ofisi ya Mbunge.

Katika harakati za kuendelea kuwafikishia viongozi wa juu wa serikali kero za wananchi wa Ngorongoro, mbunge Emanuel Shangai amesimama bungeni kuhoji kwa Waziri Mkuu sakata la uhamaji Ngorongoro ikiwa ni la hiari kwanini wananchi wanawekewa vikwanzo vya kimaendeleo?

Na Edward Shao.

Mbunge wa jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha Emmanuel Ole Shangai (CCM) ameihoji ofisi ya Waziri Mkuu iwapo zoezi la kuhamisha wakazi wa tarafa hiyo ya Ngorongoro ni la hiari inakuwaje wanasitishiwa huduma muhimu za kimaendeleo.

Mbunge huyo amehoji hayo hii leo April 08, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati aliposimama kuchangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2024/2025.

Amesema kutoka mwaka 2022 wananchi wa tarafa ya Ngorongoro wamekuwa lock down kwa ajili ya suala la maendeleo akitaja shule 27 za msingi, lakini hakuna shule hata moja ambayo kwa sasa wanaruhusiwa kujenga ama angalau kukarabati choo huku akisema wananafunzi wanaenda kujisaidia porini pamoja na walimu wao.

Ole Shangai amesema Waziri Mkuu alienda kuzungumza na wananchi Februari 14, 2022 na alisema ni zoezi la hiari, iweje sasa wananchi wawekewe vikwazo vya kimaendeleo, hata huduma za afya zimekuwa hafifu, isitoshe pia watoto wa shule ya msingi Enduleni yenye wanafunzi wa bweni, watoto kwa sasa wanaenda kuchota maji mtoni kwa sababu wamesitishiwa huduma ya maji.

Sauti ya mbunge Shangai