Loliondo FM

Enguserosambu wagoma kutoa eneo la shamba darasa Ngorongoro

22 March 2024, 2:02 pm

Moja ya maeneo ya makazi ya wafugaji wilayani Ngorongoro,picha na mpiga picha wetu.

Wafugaji waliowengi wilayani Ngorongoro wanahitaji elimu ya ufugaji bora,wakisasa na wenye tija hivyo elimu mbalimbali ihusuyo ufugaji,na mashamba darasa ni miongoni mwa elimu hiyo.

Na Edward Shao.

Mkuu wa wilaya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo amewataka wanakijiji wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro kutoa eneo kwaajili ya kuanzishwa kwa shamba darasa kwaajili malisho bora ya mifugo yao.

Ameyasema hayo Machi 20,2024 katika mkutano wa adhara na wananchi wa kata ya Enguserosambu wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa shamba darasa kwenye kata hiyo ni kupata uhaika kwa malisho kipindi cha ukame kwa wananchi hao huku akiitaja kata ya Oloipiri ambayo tayari wamekwisha anza kufundishwa kwenye shamba darasa huku kata ya Enguserosambu wakigoma kutoa eneo la shamba darasa.

Kanali Sakulo amesema benki ya maendeleo ya Ujerumani (KFW) iliyo tayari mda mrefu kutoa ufadhili kwa mafunzo hayo ya shamba darasa na wanafikiria kupeleka elimu hiyo Kijiji kingine mradi huo,hivyo amewataka wananchi hao kutoa eneo hilo mapema.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Ni mwendelezo za ziara ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo ndani ya wilaya ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi.