Loliondo FM

PWC watumia redio kumlinda mtoto wa kike kipindi cha likizo

17 December 2023, 1:52 pm

Wadau wa kupinga ukatili wakijinsia wakiwa Katika studio za Loliondo fm, picha na Edward Shao.

Jamii za kifugaji wilayani Ngorongoro wamekuwa wakitumia kipindi cha likizo kwa wanafunzi pindi wanaporudi nyumbani kutekeleza mila na desturi kwa mtoto wa kike ambazo zimekuwa zikimkatili, Mila au matendo hayo ni kama vile kuozeshwa,mimba za utotoni,kufanyishwa kazi ngumu na hata ukeketaji.

Na Edward Shao.

Baraza la wanawake wakifugaji (PWC) ijumaa ya Disemba 15 2023 wametumia redio Loliondo fm Katika kutoa elimu kwa jamii yakumlinda mtoto wa kike na vitendo vya kikatili kwa kipindi hiki cha likizo.

Akizungumza na Loliondo fm Bi Lemuta Moisane kutoka PWC idara ya haki na uongozi wa mwanamke amesema wamefanya hivyo ili kumsaidia na kumlinda mtoto wa kike asikatishe ndoto zake kwenye likizo hii ya Desimba na hatimaye 2024 anarejea shuleni kutumiza ndoto zake.

Sauti ya bi Lemuta Moisane

Pia ametaja aina ya matendo ya kikatili wanayokutana nayo PWC kwa mtoto wa kike hasa wanafunzi.

Sauti ya bi Lemuta Moisane

Afisa elimu wilaya ya Ngorongoro bw Emanuel Sukumsi amekiri wanafunzi kulindwa wawapo shuleni Ila changamoto kubwa ni kipindi wakiwa likizo.

Sauti ya Emanuel Sukumsi

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro bw Benezeth Bwikizo amesema wanachangomoto kubwa za mimba za watoto wanaporudi kutoka likizo na kwa mujibu wa takwimu mimba zote wanazopata wanafunzi wanazipata wakiwa likizo.

Sauti ya bw Benezeth Bwikizo

Naye Dr Anjela Meipuki mganga mfawidhi hospitali teule ya Wasso ametaja aina ya wototo wanaowapokea hospitalini hapo wakiwa wametendewa vitendo vya ukatili.

Sauti ya Dr Anjela Meipuki