Loliondo FM

Waziri Biteko ataka mnada wa mifugo, bidhaa ufanyike eneo moja Ngorongoro

15 April 2024, 8:09 pm

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko kushoto, akiwa na Katibu Tawala mkoa wa Arusha kulia kwenye picha ya pamoja Ngorongoro kwenye hafla ya uzinduzi wa vituo vya kurushia matangazo TBC.picha na mpiga picha wetu.

Ni uzinduzi wa vituo vya kurushia matangazo TBC Fm na Bongo Fm hapa wilayani uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi na miongoni mwa mambo mengi yaliyozungumziwa ni pamoja na kuhusu swala la mnada wa Wasso, ushuru wa mifugo pamoja na kubomolewa kwa vibanda vya wafanyabiashara wadogowadogo mji mdogo wa Wasso -Loliondo.

Na Edward Shao.

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Mh, Dr Doto Biteko ameruhusu mnada wa mifugo Wasso-Loliondo ufanyike eneo moja na mnada wa bidhaa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma wanazo hitaji eneo moja baada ya kuuza mifugo yao.

Ameyasema hayo hii leo April 15,2024 wakati wa uzinduzi wa vituo vya kurushia matangazo Tbc taifa na Bongo fm hafla iliyofanyika uwanja wa waziri mkuu uliopo mji mdogo wa Wasso.

Dr Biteko amesema hayo baada ya mbunge wa jimbo la Ngorongoro mh Emanuel Lekishon Ole Shangai kumuomba Mh waziri kuliangalia swala la mnada wa mifugo mji wa Wasso kujitenga na mnada wa bidhaa mbalimbali hali inayowapelekea wananchi kupata shida ya huduma wanazoitaji baada ya kuuza mifugo yao.

Sauti ya mbunge

Baada ya kusema hayo Mh Dr Biteko wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja hivyo amesema sasa mnada wa bidhaa na wa mifugo ufanyike eneo moja, huku kuhusu swala la ushuru wa mifugo amesema utozwe kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Kuhusu swala la kubomolewa kwa vibanda vya wafanyabishara mji mdogo wa Wasso amesema, wote walio na viwanja vyao venye hati za aridhi waruhusiwe kuyaendeleza lakini siyo kwa wale waliokuwa kwenye hifadhi ya barabara kunyume na utaribu.

Sauti ya Waziri Biteko