Loliondo FM

Atakayehama kwa hiari Ngorongoro kupewa haki zote za msingi

28 January 2024, 4:59 pm

Baadhi ya wananchi wakijiandaa kupanda basi kuelekea kijiji cha Msomera, picha na mpiga picha

Katika mwendelezo wa wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kuhama kwa hiari kupisha zoezi la uhifadhi, hatimaye kaya zingine 118 zenye watu 818 na mifugo 3,129 wamehama kuelekea Msomera.

Na Edward Shao

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. John Mongella amewahakikishia wananchi wanaohama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi kuwa serikali imejipanga na hakuna mwananchi yeyote atakayekosa haki zake iwapo ataamua kuhama kwa hiari.

Mh. Mongella ametoa kauli hiyo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha tarehe 25 Januari, 2024 wakati akiwaaga wananchi 818 walioamua kuhama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kwenda kuishi katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ameeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa na hakuna mwananchi yeyote atakayekosa kulipwa haki zake zote zilizoanishiwa katika utekelezaji wa zoezi hilo.

RC Mongella ameongeza kuwa zoezi hilo linatekelezwa kwa kuzingatia misingi yote ya haki za binadamu ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi hao wanapofika katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Richard Kiiza amesema kumekuwa na mwamko na ari kubwa ya wananchi kujiandikisha na kutaka kuhama kwa hiari ambapo katika tukio hilo jumla ya kaya 118 zenye watu 818 na mifugo 3,129 wamehama kwenda kijiji cha Msomera.

Sauti ya kameshna wa uhifadhi