Loliondo FM

Kaya 140 zanufaika na fedha za Tasaf Ngorongoro

27 March 2024, 11:39 am

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo kulia,kushoto ni mwakilishi wa ofisi ya mkurugenzi Ndg Thomas Nade picha na mpiga picha wetu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutekeleza mradi wa mfuko wa maendeleo ya jamii – TASAF kuanzia mwaka 2000, ikiwa ni moja ya mbinu za kutokomeza umasikini ambazo pia zilisaidia ajenda ya ugatuaji wa madaraka. Katika kipindi cha 2009 – 2012, TASAF ilifanya majaribio ya uhawilishaji fedha taslimu kwa masharti – Conditional Cash Tranfer (CCT) majaribio hayo yalifanyika katika Wilaya za Kibaha, Bagamoyo na Chamwino za Tanzania bara.

Na Edward Shao

Zoezi la Uhawilishaji fedha za walengwa kaya za mpango katika dirisha la Novemba/Disemba 2023 limefanyika leo tarehe 26 Machi, 2024 wilaya ya Ngorongoro katika kijiji cha Lopolun ambapo jumla ya kaya 140 zimenufaika na fedha izo.

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mhe. Kanali Wilson Sakulo pamoja na mwakilishi kutoka ofisi ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na mratibu wa TASAF wilaya bw. Thomas Nade, wamefika katika ofisi ya kijiji cha Lopolun kata ya Olorien Magaiduru kushuhudia uendeshaji wa zoezi hilo ukifanyika, huku kiasi cha shilingi 6.7 zikitolewa kwa kaya 140.

Ikumbukwe Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi milioni 442.5 za kitanzania katika Vijiji 68 wilayani Ngorongoro kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF.