Loliondo FM

Ngorongoro yafanya vizuri ukusanyaji mapato robo ya kwanza 2023/2024

13 December 2023, 12:03 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mh Marekani Bayo, picha na mpiga picha wetu.

Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro imefanya vizuri Katika ukusanyaji wa mapato kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 Julai hadi Septemba ikikusanya kiasi cha Tsh.778,893,937 ikiwa ni asilimia 25 ya makisio ya mwaka huu wa 2023.

Na Zacharia James.

Mwenyekiti ya halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mhe.Marekani Mohamed Bayo amewataka wataalam wa makusanyo kutobweteka na mafanikio ya makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha bali wafanye kazi kwa bidii ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato ili kufikia lengo la makusanyo hali itakayo saidia kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameyaeleza hayo jumanne ya tarehe 12 Disemba 2023 katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri hio ambapo ameeleza kua halmashauri imefanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 ambayo ni Julai hadi Septemba wakikusanya kiasi cha TSh.778,893,937 kutoka vyanzo mbalimbali sawa na asilimia 25 ya makisio ya makusanyo ya mwaka huu.

Kadhalika amempongeza mkurugenzi wa halmashauri,wataalam wa elimu wakishirikiana na madiwani na wazazi na wananchi kwa ujumla kwa kupandisha kwa asilimia 8.2 kiwanbo cha ufaulu kwa wananfunzi waliohitimu darasa la saba kutoka asilimia 69.71 2022 hadi asilimia 77.9 kwa mwaka 2023 hivyo kupanda kutoka nafasi ya mwisho kwa mkoa wa Arusha hadi nafasi ya tano.

Sauti ya Marekani Bayo.

Kwa upande wake mwenyekiwa kamati ya huduma za kijamii(uchumi,ujenzi na mazingira) Mhe. Philipo G Moloi amesema kikao kilichoketi tarehe 9 Disemba 2023 ilipitia utekelezaji wa maazimio yatokanayo na kikao cha kamati hiyo kilichoketi tarehe 16 Septemba 2023 inaonyesha katika kipindi cha Julai hadi Septemba mifugo waliokufa kwa kila kata katika kipindi cha ukame cha robo ya kwanza ya mwaka ni Ng’ombe 131,945,Mbuzi 74,334,Kondoo 144,173 na Punda 3,746 wakifa kwa kukosa maji,malisho na wengine kupewa sumu,huku katika kipindi hicho mtu mmoja mkazi wa kijiji cha kirtalo akiuwawa na wanyama pori wakali tembo na mifugo 6 waliuawa na wawili kujeruhiwa na -wanyama wakali fisi katika kijiji hicho.

Sauti ya Philipo Moloi.