Loliondo FM

Mabeyo: Hifadhi ya Ngorongoro inatakiwa ibaki wazi

7 May 2024, 11:17 am

Mwenyekiti wa bodi yawakurugenzi NCAA katikati jenerali Venance Mabeyo wakati wa ukagunzi wa ujenzi wa jingo la NCAA Karatu, picha na mpiga picha.

Katika jitihada za serikali za kuhakikisha eneo la hifadhi ya Ngorongoro libaki wazi kupisha shughuli za uhifadhi,mamlaka ya hifadhi hiyo NCAA wapo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa makao makuu yao wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Na Mwandishi wetu.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya hifadhi ya Ngorongoro NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amesema wameridhishwa na ujenzi wa jengo la NCAA ambalo litakuwa makao makuu ya hifadhi hiyo.

Mabeyo ameyasema hayo baada ya kutembelea jengo hilo kabla ya kuanza kwa kikao cha bodi ya wakurugenzi NCAA kilichofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha.

Amesema eneo la hifadhi linapaswa kubaki wazi kupisha shughuli za uhifadhi ndio maana tayari baadhi ya wananchi tayari wameamia maeneo mengine hapa nchini.

Sauti ya Venance Mabeyo

Jengo hilo la makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro kwa mujibu wa Mabeyo linategemewa kukamilika mwishoni mwa nwezi Juni 2024.