Loliondo FM

Naibu Waziri Mhandisi Mahundi afanya ziara wilayani Ngorongoro

27 September 2026, 4:36 pm

Naibu Waziri wa Wizira ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na Makundi maalum Mhe Mhandisi Maryprisca Mahundi katika picha ya pamoja na maafisa maemdeleo Ngorongoro. Picha na Saitoti Saringe.

Na Saitoti Saringe

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amefanya ziara katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kikazi na kufuatilia hali ya maendeleo ya jamii wilayani humo.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Septemba 26, 2026, Naibu Waziri Mahundi amekutana na kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, ambapo amepata fursa ya kusikiliza na kufuatilia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya jamii, wanawake, watoto na makundi maalum.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mahundi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, viongozi wa maeneo husika na wananchi katika kuhakikisha makundi mbalimbali katika jamii yanapata fursa sawa pamoja na huduma zinazostahili.

Amesema ushirikiano wa wadau wote ni muhimu katika kutekeleza mipango ya maendeleo na kuimarisha ustawi wa wanawake, watoto na makundi maalum katika jamii.
Ziara hiyo pia imelenga kufuatilia utekelezaji wa majukumu na masuala ya maendeleo ya jamii katika Wilaya ya Ngorongoro, pamoja na kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi katika kushughulikia changamoto na mahitaji yanayowakabili.

Naibu Waziri Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi anaendelea na ziara yake wilayani Ngorongoro kama sehemu ya majukumu ya Serikali ya kuhakikisha masuala ya maendeleo ya jamii na ustawi wa makundi mbalimbali yanaendelea kupewa kipaumbele.

Sauti ya Mhe Naibu Waziri Mahundi