Wanafufunzi kidato cha nne watakiwa kuepuka udanganyifu
November 17, 2022, 6:29 pm
Wanafunzi wa kidato cha nne wilayani Kahama mkoani Shinyanga waliotahiniwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne wametakiwa kuepuka udanganyifu kwenye chumba cha mtihani ulioanza hii leo Novemba 14, 2022.
Wito huo umetolewa leo Novemba 14,2022 na mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga ambapo amesema mwanafunzi atakaebainika kufanya udanganyifu atafutiwa matokeo na kuwataka wasimamizi wa mtihani kuwa waadilifu.
Pia amesema wazazi watakaobainika kuwaozesha wanafunzi kabla ya wakati watachukuliwa hatua za kisheria na wanafunzi wa kike ambao wataona viashiria vya kuozeshwa watoe taarifa ili wapatiwe usaidizi.
Hata hivyo jumla ya watahiniwa 566,840 wamesajiliwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne 2022 nchi nzima.