Watatu washikiliwa na polisi Shinyanga kwa mauaji
January 17, 2025, 5:41 pm
Na Neema Nkumbi
Mwili wa Mwanamke Asha Mayenga anayekadiriwa kuwa na miaka 62 alieuawa na kuzikwa Malindi Mtaa wa Seeke Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama umefukuliwa na kutambuliwa na ndugu zake.
Tukio la kufukua kaburi limefanyika januari 17, 2025 ambapo Mwenyekiti wa mtaa wa Seeke, Christopher Robert ameeleza kuwa alipewa taarifa na wachunga Ng’ombe kuhusu tukio hilo tarehe 16 Januari, saa 11 jioni na kutoa taarifa polisi.
Mume wa marehemu Mashauri Mlekwa amesema alipewa taarifa za mke wake kupotea siku ya Jumatatu alipoenda shambani kulima na vijana wake.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akikiri kuwashikiliwa watuhumiwa watatu akiwemo mtoto wa marehemu akisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kugombea ardhi (kiwanja).