Huheso FM

Mabinti balehe wakabidhiwa vifaa vya kazi kujikwamua kiuchumi

March 11, 2025, 3:54 pm

Katibu tawala mwenye suti nyeusi Glory Absalum akikabidhi vifaa kazi kwa wasichana balehe na wanawake 281

“mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU unalenga kuboresha mifumo ya huduma salama za afya ya uzazi na kuzuia ukatili wa kijinsia, hasa kwa mabinti balehe na wanawake vijana, wakiwemo wenye ulemavu.”

Na Neema Nkumbi

Zaidi ya wasichana na wanawake vijana 700 kutoka Wilaya ya Kishapu, Tarime, Butiama na Kahama wamepewa vifaakazi ikiwa Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika Manispaa ya Kahama kwa wasichana 197 kwa lengo la kuwawezesha mabinti hao kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Aneth Mushi amesema wameweza kutambua mabinti waliosomea fani mbalimbali kama vile Ushonaji, Ususi, Mapambo, Ufundi Umeme, Magari, Bomba, Mapishi, Ukarani na Uchomeleaji. Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Glory Absalum amewashauri wazazi wa mabinti hao kuwa nyuma yao ili vifaa hivyo vikafanye kazi iliyokusudiwa na kuvitunza kama sehemu ya kukuza uchumi wa familia zao, badala ya kuviweka kama dhamana katika mikopo.

Sauti ya Neema Nkumbi akisimulia taarifa ya kukabidhiwa wasichana balehe vifaa kazi
Picha ya baadhi ya vifaa kazi vilivyokabidhiwa kwa walengwa