Dawa bandia za binadamu zakamatwa Kahama
May 27, 2024, 12:39 pm
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata pikipiki 16 za wizi na zisizo na kadi, viroba 25 vya madawa ya kulevya aina ya mirungi, Tv 01, mzani 01, redio 01, pombe ya moshi lita 20 pamoja na pakti 86 za dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 27,2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema vitu hivyo vimekamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja kuanzia Aprili 17, 2024 mpaka Mei 27, 2024 kufuatia Ushirikiana wa Jeshi la Polisi na Jamii katika kubaini na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako pamoja na Operesheni mbalimbali.
Katika kipindi hicho pia Jumla ya kes 15 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya kuvunja nyumba usiku na kuiba mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01 na kesi moja ya kumtaja mtu mchawi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.