Huheso FM

Mtoto azaliwa amevunjika mkono, wauguzi waomba fedha

May 22, 2024, 12:06 pm

Picha ya Hospitali ya Wilaya ya Kahama alipolazwa mtoto aliyevunjika mkono

Na Anas Ibrahim-Huheso Fm

Imeelezwa kuwa Sofia Budeba mkazi wa kijiji cha Nyangota katika kata ya Ngaya halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, Sofia Budeba anadaiwa kujifungua mtoto akiwa amevunjika mkono.

Akizungumza na wanahabari Sofia Budeba amesema alifika katika zahanati ya Ngaya hapo siku ya Jumamosi ambapo kabla hajajifungua aliombwa fedha na wauguzi kiasi cha shilingi elfu arobaini kwa ajili ya dawa ya kuongeza kasi ya uchungu.

Akielezea tukio hilo mume wa Sofia Budeba, ambaye ni Jumanne Mkabile amesema mke wake alijifungua salama lakini mara baada ya kubainika mtoto amevunjika mkono wahudumu walimtaka atoe kiasi cha shilingi laki moja na elfu hamsini kwa ajili ya kumhudumia mtoto.

Mkabile amesema aliwapatia kiasi hicho cha fedha na suala hilo alilifikisha kwa diwani wa kata ya Ngaya ambapo watoa huduma walirejesha fedha hizo

Sauti ya Sofia Budeba na ya mume wake Jumanne Mkabile wakizungumzia tukio namna lilivyotokea

Philip Laizer ni msimamizi wa kitengo cha watoto wachanga katika hospitali ya Manispaa ya Kahama, amekiri kumpokea mtoto huyo akiwa amevunjika mkono.

Sauti ya Philip Laizer msimamizi kitengo cha watoto wachanga hospitali ya Wilaya Kahama akizungumzia hali ya mtoto

Aidha baada ya tukio hilo kutokea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amefika katika hospitali ya Manispaa ya Kahama alipolazwa mtoto huyo baada ya kuhamishwa kutoka kituo cha afya Ngaya huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wanasiasa kuacha kutumia matukio kwa maslahi ya kisiasa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha akizungumzia tukio hilo huku akisisitiza wanasiasa kutokutumia matukio kwa masilahi yao

MWISHO