Madiwani Manispaa ya Kahama waiomba halmashauri kutenga bajeti ya barabara
August 5, 2022, 5:59 pm
Madiwani wa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameiomba halmashauri kutenga bajeti ambayo itasaidia kurekekebisha miundo mbinu ya barabara zilizopo katika kata ili kupunguza changamoto hiyo kwa wananchi.
Wameyasema hayo leo katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa mkoani humo na kueleza kuwa endapo bajeti inaruhusu wanatakiwa wanunue magereda ambayo yatasaidia kurekebisha barabara hizo.
Aidha ,madiwani hao wamesema Mamalaka za barabara mjini na vijiji TARURA waanze kuzitambua barabara hizo na endapo bajeti itaruhusu zirekebishwe ili kupunguza changamoto kidogo sehemu amabzo ni korofi.
Kwa upande Meneja wa Mamlaka ya Barabara Mjini na Vijijini Joab Mtagwaba amesema wanatekeleza barabara kulingana na bajeti iliyotengwa hivyo bajeti ya barabara za mitaa haijatoka mpaka bajeti ya mwaka wa fedha ujao.
Hata hivyo changamoto ya barabara zilizopo katika mitaa manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga imekua changamoto kubwa hasa kwa kipindi cha masika.