DC Kiswaga: Maonesho ya kibiashara Kahama kuwa ya mfano
July 19, 2021, 7:42 pm
Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Festo kiswaga amewaomba wananchi wilayani humo kujitokeza katika maonesho ya Ujasiliamali na wafanybiashara wakubwa na wadogo katika viwanja vya halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani humo.
Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake amesema ulinzi na usalama umekamlilika hivyo ni matumaini yake kuwa wananchi watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kujitunza, kununa na kufanya Biashara kwani maonesho hayo yataanza July 30 hadi Agosti 8, 2021.
Mkuu wa Wilaya Kiswaga amesema tukio hilo la kibiashara na uwekezaji litachukua siku kumi na wafanyabiashara wote wanaalikwa katika maonesho hayo makubwa na ya kimfano katika mkoa wa Shinyanga.
Amesema katika Kipindi chote hicho cha maonesho wananchi wameombwa kuchukua tahadhali ya kujikinga na wimbi la tatu la Corona ambalo limekuwa kubwa na Kali huku akiahidi amekwishaandaa mazingira mazuri ya watu kunawa katika maonesho hayo na kuvaa barakoa na njia zingine muhimu za kujikinga na maambukizi ya Corona.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amesema yatakuwa maonesho mazuri na yakuvutia na hakusita kuwakaribisha watu kutoka mikoa mingine kuja katika maonesho hayo ili wajifunze.