Wananchi wahofia Magonjwa ya mlipuko baada ya uchafu kukithiri mtaani.
April 16, 2021, 3:26 pm
Wananchi wa Mtaa wa Igembensabo Kata ya Malunga katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameitaka kampuni ya uzoaji wa uchafu majumbani kufuata ratiba ya kuondoa uchafu huo ili kuepusha magonjwa ya milipuko kwa kipindi hiki cha Mvua.
Wito huo umetolewa mapema hii leo na wakazi wa mtaa huo wakati wakizungumza na HUHESO FM baada ya wakusanyaji wa uchafu kushindwa kufuata ratiba ya uzoaji kwa muda mrefu na kusababisha mrundikano wa takataka kwenye makazi.
INSERT WANANCHI……………………….
Kwa upande wake afisa wa usafi wa Manzigira wa Manispaa ya Kahama, Johanes Mwebesa amesema kampuni ya usombaji taka huwa inatumia magari hivyo gari moja iliharibika na kampuni hiyo kubaki na gari moja ambayo ndio ilikuwa inahudumia mitaa yote.
INSERT MWEBESA………………………..
Hata hivyo Mwebesa amesema gari ya pili tayari vifaa vyake vimeletwa hivyo baada ya matengenezo kukamilika ratiba ya usombwaji taka katika mitaa itarejea kama ilivyokuwa mwanzo.