Manispaa ya Kahama yapanga bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022
April 8, 2021, 3:21 pm
Halmashauri ya Manisapaa ya Kahama mkoani Shinyanga inatarajiwa kutenga bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 jumla shilingi milioni 900 hadi Billioni moja kwa ajili ya vikundi vya maendeleo kwa akina mama vijana na watu wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa idara kitengo cha maendeleo Manispaa ya Kahama, Robert Kwela wakati akizungumza na Huheso fm ofisini kwake na amesema lengo la kutoa mikopo hiyo ni kuleta ustawi wa maisha hasa akinamama.
Kwa upande wake Rehema Joshua akiwakilisha kikundi cha walemavu na mandeleo kilichopo Kata ya Malunga amesema fedha hizo zimemsaidia katika biashara zake na kusomesha watoto wake.
Hata hivyo halmashauri ya Manispaa ya Kahama kila mwaka kwenye bajeti yake hutenga bajeti kwa ajili ya vikundi vya Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambavyo hukopeshwa bila riba.