Radio Jamii Kilosa

Siku ya usafi duniani Kilosa yafanya usafi sokoni

20 September 2024, 9:29 pm

Viongozi na wananchi wakifanya usafi katika soko la sabasaba lililopo Kilosa. Picha na Stamius Kyombo

Siku ya usafishaji Duniani huadhimishwa kila ifikapo 20 Septemba ya kila mwaka huku maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo, “Uhai hauna mbadala, tuzingatie usafi wa mazingira”.

Na Asha Madohola

Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kusafisha mazingira yao mara kwa mara ili kuepuka madhara yanayotokana na uchafuzi wa mazingira.

Mkuu wa divisheni ya mipango na uratibu Ndg Wapa Mpwehwe

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Wapa Mpwehwe katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani ambayo Kiwailaya imeadhimishwa kwa kufanya usafi katika soko la Sabasaba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Ndg. Mpwehwe amewataka wakazi wa kilosa kusafisha mara kwa mara mazingira yao ya nyumbani pamoja na maeneo wanapofanyia shughuli zao huku akiwataka wananchi kufanya usafi wa pamoja kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Sauti ya Mkuu wa divisheni ya mipango na uratibu Ndg Wapa Mpwehwe

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo Kilosa Grace Chogogwe na Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Hussein Fadhili wameutaka uongozi wa soko hilo kuweka utaratibu wa kusafisha soko hilo mara kwa mara.

Sauti ya Mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo Kilosa Bi Grace Chogogwe
Diwani wa Kata ya Kasiki Mhe Ramadhan Mpangachuma

Naye Mhe Diwani wa kata ya Kasiki Mhe. Ramadhani Mpangachuma na Diwani wa kata Mbumi Mhe. Shabani Maringo Wameushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa Kuratibu zoezi hilo la usafi ndani ya soko la Sabasaba.

Sauti za Waheshimiwa Madiwani