Radio Jamii Kilosa

Kilosa wahimiza lishe kwa watoto

19/03/2026, 15:33

Afisa Lishe Bi Martha Damiano akizungumza na wanahabari ofisini kwake. Picha na Faidha Adamu

Watoto walio chini ya miaka mitano wanahitaji chakula chenye lishe bora ili kusaidia ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili ambayo husaidia kuzuia udumavu, magonjwa yanayotokana na upungufu wa virutubisho.

Na Asha Madohola

Wananchi wilayani Kilosa wametakiwa kuhakikisha watoto walio chini ya miaka mitano wanapatiwa chakula chenye lishe bora ili kusaidia ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili. Wito huo unalenga kujenga kizazi chenye afya njema na uwezo wa kuchangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Bi. Martha Damiano, wakati akizungumza na Redio Jamii Kilosa ofisini kwake na kwamba lishe bora kwa watoto ni msingi muhimu katika kuzuia udumavu na magonjwa yanayotokana na upungufu wa virutubisho mwilini.

Bi. Martha ameeleza kuwa, wamefanikiwa kutoa elimu hiyo katika kliniki ya mama na mtoto Kilosa ambapo, watoto walio chini ya miaka mitano walipatiwa chanjo na kupimwa hali ya lishe, huku wazazi na walezi wakipata fursa ya kufundishwa namna sahihi ya kuandaa chakula cha ziada kuanzia mtoto anapotimiza miezi sita.

Sauti ya Afisa Lishe Bi Martha Damiano akizungumza

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wazazi na walezi kuzingatia makundi yote sita ya vyakula ili kuhakikisha mtoto anapata virutubisho vyote muhimu huku akiwataka kuacha tabia ya kuwapa watoto uji usio na mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali.

Sauti ya Afisa Lishe Bi Martha Damiano akizungumza