Radio Jamii Kilosa

Habari za uongo,kikwazo kwa biashara Kilosa

24 November 2025, 1:26 pm

Duka la vyakula ambavyo huathirika na taarifa za uongo kuhusu bidhaa zake. Picha na mtandaoni

Habari za uongo zimekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya biashara, hasa katika jamii zinazotegemea taarifa sahihi kufanya maamuzi ya ununuzi na uuzaji.

Na Aloycia Mhina

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Kilosa, Ndugu Joshua Chaluza Mbarikiwa, ametoa wito kwa wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kuwa waangalifu dhidi ya taarifa za uongo zinazoweza kuathiri shughuli za kibiashara.

Amesema ni muhimu kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa uaminifu na kuepuka kueneza au kuathiriwa na uzushi unaoweza kupotosha soko au kuharibu taswira ya bidhaa na huduma.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Kilosa, Ndugu Joshua Chaluza Mbarikiwa, akizungumza katika makala iliyoandaliwa na Redio jamii Kilosa

Aidha, amewataka wateja kuwa makini na kuepuka kusikiliza au kusambaza habari za uongo zinazohusiana na bidhaa au wafanyabiashara, kwani jambo hilo linaweza kusababisha hofu isiyo ya lazima na kushusha kiwango cha biashara.

Mwenyekiti huyo amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa uaminifu kati ya wafanyabiashara na wateja ili kukuza uchumi wa ndani na kujenga jamii inayojali ukweli na maendeleo.