Radio Jamii Kilosa

Tasaf yafikia awamu ya mwisho Kilosa

8 October 2025, 7:39 am

Mratibu wa Tasaf Kilosa Dedan Maube akiwa katika studio za redio Jamii Kilosa. Picha na Epifanus Danford

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Wilaya ya Kilosa umekamilika Septemba 30, 2025 kwa awamu ya tatu, ukiwanufaisha wanufaika 35,756 kutoka kaya 8,834.

Na Aloycia Mhina

Mpango wa kunusuru Kaya Maskini {TASAF} Wilayani Kilosa imekamilisha utekelezaji wa Mpango huo kwa kipindi cha miaka Mitano ya Mwisho Mwezi Septemba 30 2025 kwa awamu ya tatu na kuweza Kufikia kaya 8834 ambapo ndani yake yenye wanufaika 35,756 wameweza kunufaika kwa kupata Ruzuku za kifedha na utekelezaji wa miradi ya ajira za muda katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Kauli hiyo ilitolewa Oktoba 7, 2025 na Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Wilaya ya Kilosa Dedan Maube wakati akizungumza katika Kipindi cha Ijue Halmashauri yako Radio Jamii Kilosa .

Maube alisema kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ukiwa na awamu tofauti kwa kutekelezwa kwa vipindi vya miaka mitano mitano ambapo ulianza 2014 ambapo utambuzi ulifanyika 2015 malipo yalianza kwa walengwa waliotambuliwa kwa kuvifikia vijiji kwa aslimia 70 na mwaka huu 2025 Tarehe 30 mwezi Septemba na kukamilisha mpango huo kwa kufikia kaya 8834 zenye wanufaika 35,756 mpaka kuhitimishwa mpango huo wa Tasaf.

Sauti ya Mratibu wa Tasaf Kilosa Dedan Maube

Sambamba na hayo alisema katika kipindi hiki cha miaka mitano ya mwisho wa Mpango huo wa Tasaf kulikuwa na ajira za muda ambapo miradi mbalimbali iliweza kutekelezwa na walengwa hao kupata ajira za muda na viijiji kunufaika, na uanzishwaji wa vikundi vya kuweka akiba kukuza uchumi na jumla ya vikundi 699 katika vijiji 138 Wilayani Kilosa.

Sauti ya Mratibu wa Tasaf Kilosa Dedan Maube