Mfumo wa ruzuku wapunguza gharama za kilimo Kilosa
Mfumo wa ruzuku wapunguza gharama za kilimo Kilosa
24 June 2025, 11:36 pm
Mkulima mnufaika na mfumo wa ruzuku ya pembejeo Bakari Somboja akiendelea na majukumu yake. Picha na Beatrice Majaliwa
Wakulima wanahimizwa kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku ya mbolea na mbegu ili kunufaika na pembejeo bora kwa bei nafuu. Mfumo huo unalenga kuwainua wakulima kiuchumi kupitia kilimo cha kisasa chenye tija.
Na Beatrice Majaliwa
Wakulima mbalimbali kutoka wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wameeleza jinsi mfumo wa usajili wa ruzuku ya mbolea na mbegu unavyowawezesha kupunguza gharama za uzalishaji na kuwasaidia kuongeza tija katika kilimo.
Wakizungumza na Redio Jamii Kilosa, baadhi ya wakulima waliotoa ushuhuda ni pamoja na Bakari Somboja kutoka Kata ya Mabwerebwere ambaye amesema mfumo huo umekuwa msaada mkubwa kwao, na kuwashauri wakulima wengine wasisite kujisajili ili nao wanufaike.
Mkulima Bakari Somboja akiwa bustanini
“Kupitia mfumo huu, mkulima anapata pembejeo kwa bei nafuu, jambo ambalo linapunguza mzigo mkubwa katika shughuli za kilimo,” alisema Somboja
Sauti ya mkulima Bakari Sombojo
Mkulima Bi Semeni Ally
Naye Semeni Ally kutoka Kata ya Tindiga amesisitiza kuwa mfumo huo ni mkombozi kwa wakulima wadogo.
Ameeleza kuwa kwa miaka ya nyuma walikuwa wakikumbwa na changamoto ya kupanda mazao kwa kutumia pembejeo zisizo na ubora, lakini kupitia mfumo huu wanaweza kupata mbegu bora na mbolea inayofaa kwa mazingira yao.
Sauti ya mkulima Semeni Ally Afisa Kilimo na Mratibu wa pembejeo Kilosa Juma Mihenga
Kwa upande wake, Afisa Kilimo na Mratibu wa Pembejeo wilayani Kilosa, Bwana Juma Mihenga amesema kuwa mfumo huu ni fursa ya kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo wilayani humo.
Sauti ya mratibu wa pembejeo Juma Mihenga akizungumza
Mihenga ameongeza kuwa mkulima yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na aliye na namba ya NIDA anastahili kusajiliwa kwenye mfumo huo. Amesisitiza kuwa usajili huo ni njia muhimu ya kuhakikisha wakulima wanapata huduma stahiki na zenye ubora kutoka serikalini.