Radio Jamii Kilosa
Radio Jamii Kilosa
26 May 2025, 11:40 pm

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni mpango wa kitaifa unaolenga kuwapatia wananchi elimu na huduma za kisheria bila malipo, hasa kwa wale wasioweza kumudu gharama za mawakili.
Na Beatrice Majaliwa
Wananchi wa Wilaya ya Kilosa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mikutano ya kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, inayolenga kutoa elimu ya haki na sheria kwa wananchi. Wito huo ulitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii, Saimon Silvester, alipokuwa akizungumza na Redio Jamii Kilosa kuhusu kampeni hiyo ambayo imefikia kata 19 wilayani Kilosa.
Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili kupata haki zao kupitia huduma za msaada wa kisheria alisisitiza Sylivester.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii, Mladiga Lubela, amesema kuwa kampeni hiyo imesaidia sana wananchi ambao hawana uwezo wa kifedha kupata ushauri wa kisheria na msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali kama migogoro ya ardhi, mirathi, na ukatili wa kijinsia.
Lubela ameongeza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote, bila kujali hali yao ya kiuchumi.