Radio Jamii Kilosa

Wakunga wa jadi waacheni akinamama wajawazito

10 September 2024, 12:34 am

Wanawake wametakiwa kuwa na utaratibu wa kujifungulia katika vituo vya afya na hospitalini na kuachana na mila na desturi ya kujifungulia nyumbani kwa wakunga wa jadi .
Hayo yameelezwa na Maria Chalalika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mila na desturi zinavyoathiri afya ya uzazi kwa vijana wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Amesema kuwa katika kipindi cha nyuma katika kabila lao ilikuwa wanawake wanajifungulia nyumbani kutokana na kutokuwa na elimu ya afya ya uzazi kwani ilipelekea mama akijifungua mwanaume hakuruhusiwa kumwona mke wake ambapo amesema madhara ya kujifungulia kwa wakunga wa jadi ni mengi.

“Akina mama nawashauri mhuhudhurie kliniki pindi mnapojitambua kuwa ni wajawazito na kuachana na masuala ya mila na desturi zinazopelekea mama kujifungulia majumbani” alisema Bi Maria.

Sauti ya Bi Maria Chalalika
Bi Astrida Kikudo

Naye Astrida Kikudo Mtoa Huduma za Afya ngazi ya Jamii katika Kata ya Magomeni alisema mila na desturi kwenye suala la ukeketaji lipo Serikali iingilie kati ili kukomesha vitendo hivyo kwa sababu watu wanapoteza maisha.

Sauti ya Bi Astrida Kikudo

Kwa upande wake Mwajabu Omari [18] mkazi wa kata ya Mabwebwere amesema baadhi ya familia hazioni umuhimu wa kuzifikia huduma za afya wakiwa pamoja hii ni kutokana na mila na desturi zinazomfanya mwanamke pekee ndiye mwenye jukumu la kuzifikia huduma za afya.

Sauti ya Bi Mwajabu Omary