Klabu za mchakamchaka kuimalisha uchumi Kilosa -M/Kiti Chabu.
26 January 2022, 4:03 pm
Vilabu vya mbio za mwendo pole alimaarufu Mchakamchaka Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro vimetakiwa kuweka mikakati ya kiuchumi na kuwahamashisha wanachama wake kujiunga na bima za Afy kama vile CHF Iliyo boreshwa na bima ya Mkono wa pole zitakazo wasaidia nyakati za matatizo ya ugonjwa,ulemavu wa kudumu na kifo.
Hayo yamesemwa Januari 23 mwaka huu na Mwenyekiti wa Kilosa Jogging Club Hemedi Chabu katika viwanja vya Kituo Cha Afya Kidodi wakati wa kuhitimisha mazoezi ya pamoja kati ya Kilosa Jogging Club na Kilombero Jogging club,yaliyofanyika Kata ya Ruaha Wilayani Kilosa Kwa kukimbia mbio za mwendo wa pole zaidi ya kilometa 15.
Chabu amesema kuwa Kilosa Jogging club kufanya ziara katika kata ya Ruaha lengo ni kukutana na Kilombero Jogging club kwa ajili ya kufanya mazoezi ya pamoja ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza madhumuni ya kuanzisha Kilosa jogging club ni kwamba kufanya mazoezi ya mbio za mwendo pole,mazoezi ya viungo kuhamashisha michezo mbalimbali katika Wilaya ya Kilosa , kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na Kufanya usafi wa mazingira , kutunza mazingira kwa kupanda miti,kuchangia damu,kuhamashisha wanachama wa jogging na jamii Kwa ujumla kujiunga na bima za afya na kushiriki mapambano dhidi ya uviko-19 kwa kupata chanjo.
Aidha ameongeza kuwa awali kulikuwa na club nyingi za Jogging wilayani humo lakini zimekufa kutokana na kukosa usimamizi na mipango endelevu ya kiuchumi hivyo hazina budi kujifunza kwa club zilizo simama imara kama Kilosa jogging club ambayo inajiongoza kwa mujibu wa katiba.
Amesema kuwa kufanya ziara ni utamaduni na taratibu za club hiyo toka ilipo anzishwa mwishoni mwa mwaka 2021 ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Halmashari ya Wilaya Kilosa chini ya Mh Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majidi Mwanga kutaka Kila kata kuanzisha club ya mbio za mwendo pole kwa ajili ya kuhamasisha michezo, kujihimarisha kiafya na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii .
Amewaaasa Kilombero jogging clab kuhamashisha jamii kujiunga na clab hiyo kwa lengo kuimarisha afya kwani Kata ya Ruaha inawatu wengi na vipaji mbalimbali hivyo wanajukumu la kuunganisha jamii katika clab hiyo Ili kuwa na uwanda mpana wa kujadili maswala mbalimbali ya Michezo, Afya na uchumi.
Naye Mratibu wa Kilombero Jogging club Baraka Mwambene ameeleza kufurahishwa na ujio wa club hiyo kwani wamewapata hamasa kubwa na wamehamasika hivyo watajipanga kwa ajili ya kufanya ziara Kukutana na Kilosa jogging Club kwa ajili ya kuendeleza umoja huo.
Kwa upande wake Afisa mtendaji Kata ya Ruaha Fedriki Majele amewaomba viongozi wa Serikali wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa kuzipa sapoti Club hizo ili ziweze kufanikisha malengo yao kwani ndio daraja katika kuibua vipaji na kukuza michezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Hata hivyo Majele amewashauri watumishi wote walioko kazini na walio stafu Kujiunga katika clab hizo Kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo yatawafanya kuimalisha viungo vyao na kuonekana wenye nguvu na kuepuka magonjwa ya uzeeni.
Kilosa Jogging Club ambayo imeanzishwa mwishoni mwa mwaka 2021 ambayo inawanachama zaidi ya 170 na kwamba imekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi siku ya jumamosi na jumapili na kufanya Ziara katika kata mbalimbali ambapo Desemba 18 ,2021 Kata ya Kimamba, Januari 8 2022 kata ya Dumila na Januari 23 2022 kata ya Ruaha ambako baada ya mazoezi ya viungo kulifanyika zoezi la kuchanja chanjo ya Uviko 19 , usafi wa mazingira Kituo cha Afya Kimamba , Soko kuu la Kimamba Soko kuu la Dumila na kuongeza kuwa awali Kilosa Jogging Club imekuwa ikishiriki shughuli za usafi katika Hospitali ya Wilaya Kilosa , Soko la Mjini ,eneo la Soko la Sabasaba na maeneo mengine ya mji katika kata ya Mkwatani Kasiki na Mbumi Wilayani humo.