Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya Kilosa lapitisha bajeti ya shilingi bilion 66.2
18 February 2021, 12:14 pm
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa pamoja limepitisha bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 66,286,660.980.70 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wake wa matumizi katika sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka 2021/2022.
Akisoma taari ya mpango wa bajeti katika baraza la Madiwani Februari 17 mwaka huu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Afisa Mipango Wilaya Francis Kaunda wakati wa kikao maalum cha kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti hiyo ambayo itatumika kutekeleza miradi ya maendeleo , kulipa mishahara ya watumishi na matumizi ya kawaida ya uendeshaji shughuli za halmashauri.
Akiwakaribisha madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti hiyo Mwenyekiti wa baraza la madiwani Mh Wilfred Sumari aliwataka madiwani hao kujadili bajeti hiyo katika maslahi mapana ya kuiletea hamlshauri maendeleo na kupunguza kero na shida za wananchi katika maeneo yao.
Wakitoa michango yao madiwani hao kwa pamoja wamesema licha ya kupitisha bajeti hiyo wameomba kuongezwa kwa ubunifu zaidi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kupitia njia mbalimbali za kubuni vyanzo vipya vya mapato huku wakianisha vyanzo mbalimbali kama vile ushuru wa miwa, machinjio ya nguruwe, ushuru wa ngozi na vyanzo vingine ambavyo wametaka viwekewe mpango endelevu ambao utasaidia kuingiza mapato katika siku za usoni.
Naye mbunge wa jimbo la Mikumi Mh Dennis Londo amewapongeza madiwani hao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kujadili na kupitisha bajeti hiyo huku akisisitiza kufanya kazi kwa bidii na mshikamano ili kuwaletea wananchi maendeleo katika nyanja mbalimbali kwa kuzingatia miongozo, taratibu na sheria.