Prof. Kabudi akabidhi mifuko 200 ya saruji shule ya Sekondari Mabula Kilosa ili kumaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa.
30 January 2021, 6:55 pm
Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Idan Kabudi amekabidhi saruji mifuko 200 sawa na Tani kumi yenye thamani ya kiasi Cha shilingi Milioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba Viwili nya Madarasa katika shule ya Sekondari Mabula Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Akikabidhi mifuko hiyo januari 30 mwaka huu Kabudi ambaye pia ni Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa ameambatana na Afisa Mipango Wilaya Kilosa Francis Kaunda kwa Afisa Mtendaji wa kata ya Mabula amesema kuwa ameamua kutoa Fedha zake binafsi kununua mifuko hiyo lengo likiwa ni kusaidia kufanikisha ujenzi wa vyumba hivyo kwa haraka ili wanafunzi walio faulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato Cha Kwanza mwaka huu waanze masomo mapema Mara baada ya ujenzi kukamilika .
Kabudi amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidiii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kwamba atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazo wakabili.
Nae mwanafunzi aliye jitambulisha kwa jina la Elieza Richard Chibula amemshukuru mbunge wa Jimbo hilo kwa moyo alio onyesha kujitoa kuwasaidia kutatua changamoto hiyo na kumuahidi kuwa watasoma kwa bidii na
Kufaulu kwa asilimia 100 katika mitihani ya kidato Cha nne mwaka huu dhidi ya asilimi 91 ya mwaka 2020.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Mabura ambaye ndio aliye pokea mifuko kwa niaba ya wananchi wa Mabula Bwana Emmanuel Kimario amesema kuwa Msaada huo utasaidia kutatua changamoto waliyo nayo kwani shule Ina upungufu wa vyumba viwili vya madarasa ambapo ameeleza kuwa tayali wananchi wameshaanza ujenzi kwa nguvu zao na kwamba ujenzi huo utaghalimu kiasi Cha shilingi million 40 fedha itakayo tokana na michango ya wananchi.
Kimario amesema kuwa atahakikisha hadi mwezi wapili mwishoni Madarasa yatakuwa tamekamilika na mapema mwezi wa tatu wanafunzi ambao bado hawajaanza maso Masomo .
Wananchi wa kata ya Mabula Kilosa wakishusha Mifuko ya Saruji katika Gari baada ya kukabidhiwa na Mbunge Prof Kabudi.