Rc Morogoro awachukulia hatua Wenyeviti wa vitongoji Mikumi.
7 January 2021, 1:05 pm
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amekemea vikali kitendo kilichoonyeshwa na Wenyeviti wa vitongoji 21 Katika Mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi kwa kushindwa kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa Katika shule ya Sekondari Mikumi ambapo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi Ruhembe (OCD) kuwaweka ndani wenyeviti hao kwa kuonyesha lengo la kuto fanikisha Ujenzi wa Madarasa hayo ambayo yanategemewa kutumiwa na wanafunzi wanao takiwa kuanza kidato cha kwanza shuleni hapo .
Ametoa agizo hilo Januari 6 mwaka huu wakati alipokuwa Katika ziara yake Wilayani Kilosa ambapo amesema ziara yake ni katika utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa la kutaka wanafunzi wote waliofaulu Mtihani wa darasa la saba kuwa madarasani pindi shule zitakapo funguliwa Januari 11 ,2021 hivyo kila mkoa unapaswa kuhakikisha wanafunzi hawakosi vyumba vya madarasa pamoja na meza na viti vya kukalia .
loata amesema kuwa shule hiyo inatarajiwa kupokea wanafunzi 432 ambao wamepangwa katika shule hiyo ambapo ametaka kasi ya ujenzi kuongezeka na kufanya jitihada za kumaliza Ujenzi huo kadri itakavyo wezekana na kwamba hatarajii wanafunzi hao kukosa madarasa ya kusomea huku akitaka wenyeviti hao baada ya kukamatwa wafikishwe eneo la ujenzi kushiriki wao wenyewe katika kazi kwani wameshindwa kuhamashisha wananchi wao na kwamba atapita Katika eneo hilo kwa ajili ya ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hilo.